Monday, November 30, 2015
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Eunice Chiume (wa pili kulia), akiwapa maelezo kuhusu huduma
zitolewazo na NSSF wakulima wa Kijiji cha Msijute, Kata ya Mayanga,
mkoani Mtwara, kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘NSSF Kwanza’,
ambayo inaendelea kwa kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi.
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Eunice Chiume akiwapa maelezo wakazi wa kijiji cha Msijute jinsi
ya kujiunga na Huduma ya mafao ya Matibabu bure kwenye kampeni maalumu
ya kuwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara juu ya faida za Hifadhi ya
Jamii kupitia NSSF.
Wakazi
wa Kijiji cha Msijute kata ya Mayanga Mkoani Mtwara wakijiandikisha
NSSF ili kuweza kujipatia mafao bora kutoka NSSF yakiwemo mafao ya
matibabu bure kwa wanachama na familia zao.
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho
zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza
ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta
isiyo rasmi.
Kampeni hiyo yenye malengo ya kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na pia Kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.

Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.
NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.
0 comments :
Post a Comment