Na Mwandishi Wetu, Moshi
MKUU
wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika
masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu,
ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika
ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake,
hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko
lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara
ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa
huo.
Akizungumzia
ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya
Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala
linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa
hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika
katika suala zima la usafi.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea
na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro
kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
“Pamoja
na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona Mkoa wetu wote
unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka kwa wakati,
uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa Hospitali ya
Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema Makalla. Kwa mujibu
wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika mazingira ya uchafu si
tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia itazalisha ugonjwa wa
mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika kuweka katika kambi
katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla akipata maelekezo kutoka kwa watendaji na watumishi katika Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika sehemu mbalimbali kwenye manispaa hiyo. Bashir Nkoromo 15:27 (40 minutes ago) to Kambi, Josephat, pamojapure, othmanmichuzi, me, muhidinuk, josephat.lukaza, cathbert39, zainul.mzige21, fadhiliathuman., amichuzi, assengaoscar, dande15us Mbwana, kwa nini kwenye captions unaandika "Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla"? RC si ndiyo mkuu wa mkoa kwa Kiingereza? Kumradhi, imebidi nikuambie kwa sababu umeirudia sana. Zaidi ya hapo nakutakia kazi
0 comments :
Post a Comment