Monday, November 30, 2015
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea
wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa
wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja
vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na
kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
Baadhi
ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu
wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume
wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa
wanawake lililoandaliwa na FIFA.
Mabalozi
walioteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini
wakijitambulisha kwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Live Your Goals
lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume kwa mara
ya pili baada ya kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza Mkoani Geita
mnamo mwezi Julai 2015.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (wapili kushoto) akimwangalia mtoto Zaynab Dotto mwenye umri wa
miaka 10 anavyocheza na mpira kwa umahiri jana jijini Dar es Salaam
katika Viwanja vya Karume. Kulia ni Mratibu wa Michezo ya Vijana wadogo
Bw. Raymond Gweba na kushoto ni mama mzazi wa mtoto Zaynabu Bibi. Pili
Said.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka
FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha
mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (watatu kushoto) akitoa zawadi ya mpira kwa mwanasoka wakike
kutoka shule ya msingi Kingugi walioshiriki katika tamasha la Live Your
Goals linalo hamasisha mpira wa miguu wa wanawake jana jijini Dar es
Salaam katika Viwanja vya Karume.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na
wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira
wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals
lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (watatu kushoto) akisisitiza jambo jana alipokutana na timu ya
taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kuikabidhi bendera ya taifa
kabla ya kwenda nchi mbalimbali za afrika kwa ajili ya mazoezi ya
kujihimarisha kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17
mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kulia) akikabidhi bendera ya taifa kwa naodha wa timu ya taifa
ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 Bw. Issa Abdi jana katika Viwanja
vya Karume kwa ajili ya kwenda nchini Rwanda, Uganda na Kenya kupata
ujuzi na mazoezi kabla ya kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya
Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.
0 comments :
Post a Comment