Nkupamah media
Taswira
za shughuli malumu ya chakula cha mchana iliyofanyika pale Courtyard
Protea hotel ya Sea View jijini Dar es salam kwa ajili ya wazee
wasiojiweza wanaosaidiwa na Asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation siku
ya Jumamosi tarehe 19 Desemba, 2015.
Shughuli
iliandaliwa na uongozi wa Protea na Rickshaw kwa ajili ya kusherehekea
Krismas na mwaka mpya. Jumla ya wazee 60 na wajukuu wao
walikaribishwa na kusaidiwa na wafanyakazi
wa Protea. Viongozi pamoja na wahudumu waliopokea
wageni wao kwa kujituma na uchangamfu mkubwa.
Mmoja wa wazee akisaidiwa kupelekwa mezani
Mmoja wa wazee hao akisaidiwa kuketi
Bibi akiongozwa kuketi
Pasina kujali nyadhifa zao mafisa wa Courtyard Protea hotel walisaidiana na wahudumu kuhudumia wazee hao kwa furaha na upendo
Bibi akisaidiwa kuketi mezani
Mwenyekiti wa TPF Mama Rose Mwapachu akikawashukuru Viongozi na
wafanyakazi wa Protea na Rickshaw kwa shughuli hiyo iliyofana sana
Asante sana mwanangu...anaonekana kusema bibi huyu wakati akiandaliwa chakula
Mzee Hashim Ismail Mkurugenzi mkuu wa Protea akimsaidia Mzee
Mchopa asieona.
Sister kutoka Msimbazi Kijiji cha wazee nae alikuwepo
pamoja na wazee kutoka Kijiji hicho.
Mmoja wa wazee akiendelea kupata vinywaji na chakula
Zawadi zilitolewa kwa wazee hao
Mama Mariam akitoa zawadi kwa wazee
![]() |
Wakurugenzi wa Protea
wakifurahia kula pamoja na wazee |
0 comments :
Post a Comment