Wednesday, December 2, 2015
@nkupamah blog
Baada ya agizo la Rais John Magufuli kutembelea
hospitali ya Taifa Muhimbili..aliagiza badhi ya mambo kufanyiwa
utekelezaji ikiwemo mashine za CT Scan na MRI ambazo zilikuwa na
matatizo kutengenezwa ili kuwasaidia wagonjwa.
Leo Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Donan Mbando
ametembelea hospitali hiyo na kukagua maeneo mbalimbali na kuzindua
duka la dawa la MSD pamoja na kukagua mashine za CT Scan na MRI ambazo
kwa sasa tayari zimeanza kufanya kazi kama kawaida.
Mengine
kutoka katika taarifa yake Mbando amesema kumekuwa na changamoto ya
kuwapeleka wagonjwa wengi nje ya nchi ikiwemo wa moyo, figo na saratani
lakini kama Serikali wamejitahidi kuhakikisha wanajenga uwezo wa
kuhakikisha huduma hizo zinapatikana ndani ya nchi.
Wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi sasa kutibiwa ndani ya nchi... “Hawa
wagonjwa tungewapeleka nje tungetumia zaidi ya milioni 500, mwaka huu
tumetenga bajeti bilioni 5 ya kuwaleta wataalam kuja kufanya kazi hapa
ili kupunguza gharama ya kusafirisha wagonjwa, mfano sasa hivi
ukitembelea India kwa sasa wagonjwa wengi ambao walikuwa wakipelekwa
huko wamepungua sana, na itafika wakati kutakuwa hakuna kabisa wagonjwa
kwenda kutibiwa nje”…Donan Mbando.
Watalamu wa mafunzo kutoka Marekani tayari wamewasili nchini..”Kuna
wataalamu kutoka Serikali ya Marekani ambao tayari wamewasili na kutoa
mafunzo itasaidia kupunguza gharama kupeleka wagonjwa nje ya nchi,
tungewapeleka nje ya nchi tungetumia milioni 500, tulitenga bajeti
bilioni 5 bajeti ya mwaka huu kwa kuleta wataalam kuja kufanya kazi
hapa, naamini tunapojenga uwezo kwa wataalam wa hapa nyumbani itasaidia
kupunguza gharama..
Kuhusu deni la mashine za MRI na CT Scan Mbando aliongeza kuwa… “Haiingii
akili ninakupa kifaa kinakuingizia mapato bado unataka Serikali itoe
fedha za matengenezo, tumetoa amelekezo kuwa baadhi ya mapato yatengwe
kwa ajili ya kutengeneza vifaa tiba.
"Kila
hospitali za Mikoa na kanda zitenge bajeti ya kutengeneza vifaa vyao,
mfano una mashine inayokutengenezea kiasi cha milioni 100 kwa mwezi bado
unataka mtu mwingine atoe pesa yake kukutengenezea kifaa hicho, siyo
sahihi?…Serikali imenunua vifaa tiba kwa ajili ya kutoa huduma kwa
hospitali zote nchini.
Kuhusu deni la MSD Mbando alisema..."Tunatakiwa
kama Serikali kuchangia bilioni 10, tumelipa milioni 42 na tumeweka
programu maalumu ya mapokezi ya dawa kwamba kila anayetaka kutusaidia
msaada wa dawa ziwe hazijapungua matumizi kuanzia miezi sita na
kuendelea, deni lililobaki tutaendelea kulilipa kwa utaratibu, jumla ya
deni tunalodaiwa ni zaidi ya bilioni 120 lakini lililohakikiwa na
mkaguzi mkuu wa Serikali ni bilioni 53 na tutaliingiza kwenye bajeti
yetu”…Mbando.
Taarifa ya mashine za CT Scan na MRI kuanza kufanya kazi.Mkuu wa Idara ya Radiologia Flora Lwakatare amesema.. “Tumeanza
kutumia mashine hizo baada ya kufanyika matengenezo na tayari jumla ya
wagonjwa 76 wametumia mashine ya MRI huku wagonjwa 152 wakiwa
wameshatumia mashine za CT Scan”..Lwakatare
0 comments :
Post a Comment