NA BASHIR YAKUB -
WAPO
mawakala na wapo wanaohitaji kuwa mawakala, Kwa sasa biashara ya
uwakala ni kubwa mno, wapo mawakala mitandao ya simu kama tigo,
Airtel, voda n.k, mawakala makampuni ya usafirishaji kama mabasi,
malori n.k , na makampuni mengine mengi. Mtindo wa biashara ya
uwakala umekua sana katika siku za hivi karibuni.
Ni
kutokana na ongezeko la makampuni na kukua kwa biashara, Upo
umuhimu mkubwa wa kuijua biashara ya uwakala kwa undani hasa
katika misingi ya kisheria .
Hii
itakusaidia kuzijua haki zako, usipozijua haki zako za kisheria
katika biashara kama hii ni vigumu kunufaika. Hii ni kwasabbu
hutojua unastahili nini na nini hustahili. Ili kuliepuka hili
unajikuta katika ulazima wa kuzijua taratibu za kisheria
zinazohusu uwakala. Usiingie katika biashara hii bila kujua japo
mambo kidogo ya msingi ya kisheria yanayohusu uwakala.
1.WAKALA NI NANI.
Sura
ya 345 kifungu cha 134 cha sheria ya mikataba kinaeleza nini
maana ya wakala. Kinasema kuwa wakala ni mtu aliyeajiriwa
kufanya kazi au kitu chochote kwa niaba ya mwingine au
kumwakilisha mtu mwingine katika shughuli fulani. Kwahiyo wakala
ni mtu anayesimama badala ya mtu mwingine.
Huyo
mtu mwingine huitwa mhusika mkuu, Kwahiyo wakala hufanya kazi kwa
niaba ya mhusika mkuu, Humwakilisha mhusika mkuu.
2. SIFA ZA KUWA WAKALA.
Vifungu
vya 135 na 136 vinaeleza sifa za mtu kuwa wakala au kuwa
mhusika mkuu, Vinaeleza kuwa mtu yeyote mwenye umri wa mtu
mzima yaani mwenye umri wa miaka 18 na kwenda mbele anaweza
kuwa wakala.
Lakini
pia ni lazima awe na akili timamu, Kwa sifa hizi pia
unaweza kuwa mhusika mkuu,,hata hivyo hizi ni sifa za jumla za
kisheria, yamkini zipo sifa nyingine kutegemea na mhusika mkuu
anahitaji wakala wa aina gani kwa ajili ya biashara zake.
3. MAMLAKA ALIYONAYO WAKALA.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 38 wakala anayo mamlaka makuu ya aina
mbili, Kwanza mamlaka ya kutamkwa (expres) na pili mamlaka ya
kumaanisha(implied). Mamlaka ya kutamkwa ni yale yote ambayo
ameambiwa kwa mdomo au kwa maandishi kuyatekeleza .
Ni yale yaliyo katika mkataba wake alioingia na mhusika mkuu.
Pili ni mamlaka ya kumaanisha.
Haya
hayapo katika mkataba wake na wala hakuambiwa na mhusika mkuu
lakini ameyatekeleza. Haya ni yale ambayo wakala huyatekeleza
kwa nia nzuri au kwa lengo la kuikoa biashara na jambo
fulani ambalo limetokea ama kwa dharula au vinginevyo.
Ikiwa
wakala amefanya jambo jema na kwa nia njema hata kama halipo
katika makubaliano kati yake na mhusika mkuu basi jambo hilo
huhesabika ni sehemu ya mamlaka yake na mhusika mkuu hawezi
kukataa kuliwajibikia kwa kisingizio kuwa halipo katika
makubaliano.
4. HAKI YA WAKALA KUZUIA MALIPO YA MHUSIKA MKUU.
Ikiwa
wakala anafanya biashara ambayo anatakiwa kuwasilisha pesa za
mauzo kwa mhusika mkuu na ikatokea kuwa hajalipwa malipo yake
basi anaweza kuzuia malipo ya pesa hizo ili kufidia hela
anayodai. Muhimu ni kuwa asizuie pesa nyingi zaidi kuliko kiasi
anachodai.
Pamoja
na hayo kifungu cha 172 kinasema hakutakuwa na malipo kwa
wakala kwa kazi aliyoiharibu. Wakala anatakiwa kuwa mwangalifu,
mtiifu kwa maelekezo ya mhusika mkuu, na kujiepusha na uzembe au
kutojali. Hasara anayoisababisha kutokana na haya itakatwa katika
malipo yake.
5. WAKALA KULIPWA PESA ISIYOKUWA KATIKA MAKUBALIANO.
Ikiwa
wakala amefanya jambo jema na la faida kwa mhusika mkuu basi
wakala anastahili malipo ya jambo hilo hata kama malipo hayo
hayapo katika makubaliano. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha
174 cha sheria ya mikataba.
6. FIDIA KWA KUJIONDOA KATIKA UWAKALA.
Yeyote
kati ya mhusika mkuu au wakala anaweza kujiondoa katika
uwakala. Yeyote atakayejiondoa katika uwakala kabla ya muda wa
makubaliano kuisha basi atalazimika kumlipa fidia mwingine.
Akijiondoa wakala fidia italipwa kwa mhusika mkuu halikadhalika
mhusika mkuu akijiondoa fidia italipwa kwa wakala. Taarifa ya
muda wa kutosha ni lazima itolewe kabla ya kujiondoa la sivyo
aliyejiondoa atalazimika kulipa fidia nyingine zaidi kwa madhara
yaliyotokana na kujiondoa kwake ghafla.
0 comments :
Post a Comment