Na Mahmoud Ahmad Arusha
Afisa elimu wa halmashauri ya
wilaya ya Longido, Shaaban Shemzighwa, ameyaeleza hayo kwenye kikao cha
elimu cha mkoa kilichokuwa kikipitisha majina ya wanafunzi waliohitimu
elimu ya msingi mwaka 2015,ambao wamechaguliwa kujiunga na sekondari
mwakani .
Akitoa ufafanuzi wa hoja za
wajumbe ambao walitaka kufahamu mkakati wa halmashauri hiyo kukabiliana
na utoro unaosababsha wanafunzi hasa wasichana ambao wamekuwa wakiacha
shule na kuolewa ,amesema halmashauri inaendelea na kuwarejesha
wanafunzi wote waliotoroka na kuolewa.
Amesema wanafunzi wawili ambao
walikuwa wameolewa wamerejeshwa kuendelea na masomo yao katika shule ya
msingi Kitumbeine na lengo ni kukabiliana na utoro wa wanafunzi.
Amesema licha ya utoro huo wa
wanafunzi bado halmashauri hiyo ya Longido, imezidi kaulisha wanafunzi
wengi ukilinganisha na halmashauri zingine za mkoa wa Arusha na hayo ni
mafanikio makubwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya
hiyo Ernest Kahindi, akichangia kwenye kikao hicho amesema watoto wa
jamii za wafugaji waishio maeneo yote ya mpaka na nchi ya Kenya,
wanasoma shule za Kenya.
Amesema watoto wa jamii za
wafugaji kusoma nchini Kenya ni jambo la kawaida na lbda inachangiwa na
jamii hizo kutokuishi karibu na shule hivyo inakuwa ni rahisi
kuwapeleka nchini humo kusoma.
Amesema jiografia ya wilaya za
mipakani hasa kwenye jamii za wafugaji nayo ni tatizo maeneo mengi
hayana bara bara, mawasiliano ,shule wala miundo mbinu na matokeo yake
ni kuwepo na mahudhurio hafifu shuleni.
Amesema wakati wa likizo watoto
hao hupelekwa nchini Kenya ambako huwa baadhi yao wanaolewa na hilo ni
njambo la kawaida kwa jamii za wafugaji waishio mipakani .
0 comments :
Post a Comment