Tuesday, December 1, 2015
@nkupamah blog
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, January Makamba amesema kasi ya utendaji inayooneshwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, imekipa uhai mpya chama chao na kwamba wanaCCM sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele.
Akizungumza jana na mwandishi wetu
Dar es Salaam, January alisema wakati wa kampeni CCM iliahidi
itawaletea Watanzania mabadiliko na jambo hilo ndilo hasa linalofanywa
na Magufuli na Majaliwa.
“WanaCCM
sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele na kuwapongeza Magufuli na
Majaliwa kwa kutoa matamko ya kuwaunga mkono kwa hatua wanazochukua.
Wakati wa kampeni tuliahidi mabadiliko ya kweli. Na sasa tunaanza
kuyaona,” alisema January na kuongeza:
“Tusikae
kimya. Hii ni vita kali na naamini Watanzania wote wanamuunga mkono,
lakini kwa kuwa anatekeleza ahadi ya CCM sisi tunapaswa kuwa mstari wa
mbele kwa kumuunga mkono kwa maneno na matendo.
“Tulipigana
kufa na kupona ili tushinde na baadhi yetu tunaendelea kupokea vitisho
na matusi kwa sababu ya kampeni kwa vile kwa wapinzani ushindani
haujamalizika baada ya kumalizika kwa kampeni. "
Mbunge huyo wa Bumbuli mkoani Tanga na Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kama mwana CCM na MNEC anajisikia fahari kwa vitendo vinavyofanywa na Magufuli kwa vile vimekipa chama pumzi na uhai mpya, akikumbusha maneno yaliyokuwa yakitumika na wapinzani kwamba chama hicho sasa kimeishiwa pumzi.
Mbunge huyo wa Bumbuli mkoani Tanga na Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kama mwana CCM na MNEC anajisikia fahari kwa vitendo vinavyofanywa na Magufuli kwa vile vimekipa chama pumzi na uhai mpya, akikumbusha maneno yaliyokuwa yakitumika na wapinzani kwamba chama hicho sasa kimeishiwa pumzi.
“Lazima
CCM ihakikishe Magufuli na Majaliwa wanafanikiwa katika uongozi wao.
Hapo ndiyo nguvu iliyotumika katika kampeni itakuwa na maana. Kazi
anayofanya Rais inakiletea chama pumzi na uhai mpya.
“Kwa
mwendo huu, hakutakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
kama ilivyokuwa mwaka huu. Inawezekana wapo wanaCCM watakaoguswa na
utendaji huu wa Rais, lakini hiyo ni gharama ndogo sana ya kulipa kwenye
kuitafuta Tanzania ambayo kila mwananchi anaililia,” alisema.
0 comments :
Post a Comment