Kortini kwa kuingia nyumbani kwa Mzee Mwinyi

@nkupamah blog

MKAZI wa Ilala Mtaa wa Lindi, Hafidhi Ally (23), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kuvamia kisha kuingia nyumbani kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Mbele ya Hakimu Ester Kihiyo, karani wa mahakama hiyo, Mosses Mchome, alidai kwamba mtuhumiwa alifanya kosa hilo Desemba 10, mwaka huu saa 7:30 usiku nyumbani kwa Mzee Mwinyi,  Mikocheni B, Dar es Salaam.
Karani Mchome aliiambia mahakama hiyo kwamba, Hafidhi aliingia hadi ndani ya nyumba hiyo bila ruksa kutoka kwa mlinzi aliyekuwapo kwenye lindo, Nuru Saidi, ambapo alimweleza kwamba hana mahali pa kuishi.
“Mtuhumiwa ulikaidi amri ya mlinzi aliyekuwepo zamu siku hiyo, aliyekutaka urudi ulipotoka, kisha ulisisitiza kwamba huna sehemu ya kuishi, lakini pia wewe ni mtoto wa rais huyo mstaafu wakati huo ukielekea ndani kitu ambacho ni kinyume cha sheria,” alidai Mchome.

Mtuhumiwa alikana kosa hilo na upelelezi bado unaendelea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 28, mwaka huu na mtuhumiwa alirejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo alitakiwa apeleke wadhamini wawili waaminifu wenye barua kutoka kwa ofisa mtendaji wa kata anakoishi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment