Mama Shekha Nasser Akikata Keki ikiwa ni kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Mama
Shekha Nasser aliamua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula mlo
wa jioni pamoja na wafanyakazi wake wote wakiwa na washiriki wa Manjano
Dream-makers. Ikiwa ni utamaduni wa kampuni yake kufanya sherehe ya
kuuaga mwaka alitumia kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na
wanawake Wajasiriamali wa Taasisi yake aliyoianzisha ya Manjano
Foundation ambayo amewawezesha kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na pia
kuwafundisha ulimbwende pamoja na kuwakopesha mitaji ya bidhaa za
vipodozi vya LuvTouch Manjano kufanya Biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi
hivyo pendwa Tanzania. Mama Shekha amewashukuru sana na amewaasa
wanawake hao kupambana zaidi kila kukicha kwa lengo la kila mwanamke
kufikia malengo aliyojiwekea kuwa mfanyabiashara wa kujitegemea.
Mama
Shekha Nasser akipokea zawadi mbalimbali alizotunzwa na wanawake
wajasiriamali wa Manjano Dream-makers na waajiriwa wa kampuni ya Shear
illusions. Wanawake wajasiriamali walimshukuru sana Mama shekha kwa moyo
wake wa kujitolea ambapo amewawezesha kupiga hatua kwa kugusa maisha
yao ya kila siku na pia kuwakutanisha na watu wengi wakiwemo wateja wao
na mentors. Wafanyakazi pia walishukuru na kusema walifurahi kutolewa
dinner na boss wao na kufurahia chakula cha jioni na Mama yao kwa kuwa
mara nyingi wanaonana mazingira ya kazi tu
Mama Skekha Nassea Katika Picha ya Pamoja na wateja waliomtembelea Kupata Huduma Mbalimbali .
0 comments :
Post a Comment