Kampuni
ya vifaa vya ofisi na mashuleni ya Masumin Printways na Five Star
zimeamua kudhamini kwa muda wa miezi mitatu mdahalao wa kitaaluma kwa
shule za sekondari za Dar es Salaam lengo likiwa kuongeza weledi wa
wanafunzi katika masuala mbalimbali.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mdahalo uliohusisha Shule za Sekondari za St.
Antony na Debrabant zote za Mbagala jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Masumin, Shakir Karim alisema kuwa wameamua kudhamini
midahalo hiyo ili kuinua kiwango cha ufahamu kwa wanafunzi.
Alisema
pia midahalo hiyo ambayo itakuwa kwa lugha ya kiingereza inatarajiwa
kuwasaidia wanafunzi kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza na kuchambua mambo
kwa kutumia lugha hiyo ya kigeni ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa
walio wengi nchini.
“Tunathamini
elimu na ndio maana kampuni yangu daima imekuwa ikijishughulisha na
masuala ya vifaa vya shule na maofisini” alisema na kuongeza kuwa mpango
wa sasa wa elimu bure utakuwa na manufaa kwa umma kwani kuna familia
nyingi zilishindwa kusomesha kutokana na ada na michango mbalimbali.
Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mratibu wa midahalo hiyo, Shukuru
Ngongoje alisema midahalo hiyo ambayo pia itaonyeshwa moja kwa moja na
Kituo cha Luninga cha Channel Ten, itakuwa na msaada mkubwa kwa
wanafunzi.
Alisema
wameanza na shule hizo mbili na zingine zaidi zitaongezwa kulingana na
makubalino baina yao na wamiliki wa shule ambao amewataka kumpa
ushirikiano kwa faida ya wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es
Salaam.
Mwalimu
wa taaluma katika shule ya Debrabant, Reginald Komino alisema siku za
karibuni shule nyingi zimekuwa zikikwepa kuwapeleka wanafunzi wao katika
midahalo hali ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kushuka kwa kiwango
cha elimu nchini na uwezo wa wanafunzi kujieleza.
Alisema
mratibu huyo kuwa siku za karibuni imekuwa shida kidogo kupata
wanafunzi kwa ajili ya kushiriki midahalo ya kitaaluma ya namna hiyo na
kizingizio kikubwa wanachotopa ni kuwa wapo katika program za shule zao
za kuandaa kwa ajili ya mitihani hivyio hawana muda.
Alisema
midahalo ina nafasi kubwa katika kuwajenga wanafunzi na kuwafanya
wajiamini na kuwa na uwezo wa kujieleza mbele ya wenzao na pia inapanua
ufahamu wao katikia masuala mbalimbali ambayo mengine si ya darasani.
Doreen
Masau wa shule ya sekondari ya St. Antony akishiriki katika mdahalo wa
kitaaluma ulioandaliwa na Masumon Printways na Five Star na kufanyika
jijini Dar es Salaam jana. Mdahalo huo ambao ni kwa ajili ya shule za
sekondaeri za Dar es Salaam uliihuisha pia shule ya Debrabant.
Sylivanus
Ndayisenga wa shule ya sekondari ya Debrabant, akishiriki katika katika
mdahalo wa kitaaluma ulioandaliwa na Masumon Printways na Five Star na
kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Mdahalo huo ambao ni kwa ajili ya
shule za sekondari za Dar es Salaam uliihuisha pia St Antony.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Masumin Printways, Shakil Karim (kulia),
akimkabidhi vifaa vya shule, Sylivanus Ndayisenga wa shule ya sekondari
ya Sty Antony mara baada ya uzinduzi wa mdahalo wa kitaaluma kwa
wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam, juzi. Katikati ni
mratibu wa mdahalo huo, Shukuru Ngongoje.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Masumin Printways, Shakil Karim (kulia),
akimkabidhi vifaa vya shule, Doreen Masau wa shule ya sekondari ya St.
Antony mara baada ya uzinduzi wa mdahalo wa kitaaluma kwa wanafunzi wa
shule za sekondari za Dar es Salaam, juzi. Katikati ni mratibu wa
mdahalo huo, Shukuru Ngongoje. Picha na Mpigapicha Wetu
0 comments :
Post a Comment