Msanii wa kike mwenye sauti laini na nyororo yenye kuvutia Rubby, aliyejulikana kwenye game kupitia wimbo wake wa Na Yule alioandikiwa na mwanamuziki mahiri nchini Barnaba na kumfanya
kutambulika kutokana na ujumbe wake wa kimapenzi kuwagusa wengi.
Rubby kwa sasa anatamba na nyimbo yake ya Sijutii ambayo haina muda mrefu sana kwenye masikio ya mashabiki wake,huku tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mwaka 2016 wasanii wengi hueleza jinsi watakavyo funga mwaka na kufungua mwaka,
Kwa upande wake Rubby ameeleza kuwa anampango wa kuunza mwaka kwa kuachia Album yake, ambayo hakutaja jina na kueleza ataiuza kwa njia ya aina gani kati ya Online au kutoa CD


0 comments :
Post a Comment