MKURUGENZI TBC AFUNGUKA JUU YA TBC1 KUONYESHA HARUSI LIVE.

Nkupamah media

DAR ES SALAAM

Shirika la Utangazaji TANZANIA TBC limesema halijakiuka sheria za utangazaji kufuatia kipindi  maalumu cha chareko kilichorushwa na kituo hiki Desemba 19 siku ya jumamosi na kuwa kilichofanyika ni ubunifu wa
vipindi.
Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi Mkuu wa TBC, CLEMENT MSHANA amesema mteja wa kipindi hicho alitaka harusi yake irushwe moja kwa moja ambapo pia alipewa maelekezo ya kuzingatia wakati kipindi kitakapokuwa kikirushwa.
MSHANA amesema TBC ipo tayari kupokea maoni mbalimbali ya watazamaji wake ili kuboresha utendaji kazi wa chombo hicho, ambapo amewataka watazamaji kuendelea Kutazama TBC
Hii inakuja kufuatia hivi kitendo cha shirika hilo la umma kuamua kurusha ‘live’ harusi,kitu ambacho kililalamikiwa na wadau wengi hususani watazamaji wa kituo hicho,hali iliyompelekea Waziri wa Habari,sanaa na michezo Nnape Nnauye kumtaka Mkurugenzi huyo kujieleza ni kwa nini chombo hicho cha umma kinadiriki kufanya mambo hayo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment