VIONGOZI WAPYA WA TAHLISO WAAPISHWA RASMI,


Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI juzi tarehe 29/12/2015 Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania
 
 
Uongozi mpya wa
shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo
tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi
aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu
inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti  mpya wa TAHLISO  Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo juzi jijini Dar es salaam
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika
viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS
PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina
ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mikopo kwa
wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi
wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana
na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa juzi Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti huyo amesema
kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya
Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo
na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani
neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa
serikali ya awamu ya tano.
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa juzi
Viongozi wa TAHLISO
wameapishwa juzi rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia
uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa
mujibu wa katiba yao.

JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa juzi
 
Omary Idd  Naibu muazini akiapa juzi tayari kulitumikia shirikisho hilo
 
Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini

Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo

 
Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO juzi Jijini Dar es salaam
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment