WAZIRI KITWANGA AKARIBISHWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU LEO

@nkupamah blog

kit1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
kit2
kit3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya
waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
kit4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
kit5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
kit6
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani). Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment