ZAIDI YA MITAMBO 30 YA UMEME JUA YATOLEWA MSAADA KWA JAMII

 
ZAIDI ya mitambo ya sola 30 imetolewa kwa jamii mbalimbali yenye
 uhitaji zikiwemo Zahanati ,vituo vya afya,ofisi za watendaji kata  na
 shule mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha huduma zao
 wanazotoa kwa jamii.  Hayo yalisemwa jana na Meneja masoko wa kampuni ya Sola ya  Mobisol
 ,Seth Matemu  na  Meneja Mauzo ,Joseph Zikhali wakati wakizungumza na
 waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza ofa mpya ya msimu wa
 sikukuu kwa wateja wake .
Alisema kuwa, kampuni hiyo ya sola imekuwa ikisaidia shughuli
 mbalimbali za kijamii hususani zenye uhitaji ambapo hadi sasa hivi
 wamekwisha tumia kiasi cha shs 15 milioni kwa ajili ya kusaidia
 mitambo hiyo .
 Matemu  alisema kuwa, lengo la kuwasaidia jamii hiyo ni mojawapo ya
 malengo ya kampuni hiyo kuhakikisha kuwa inarudisha sehemu ya faida
 kwa wananchi wake kwa kugawa mitambo ya sola bure kwa wenye mahitaji.
 Alisema kuwa,kampuni hiyo ina zaidi ya wateja 20,000 kwa Tanzania
 nzima ambapo wananchi wengi  kwa sasa wana mahitaji ya umeme wa jua
 kutokana na changamoto kubwa ya umeme unaokatika kila wakati na hivyo
 kuchangia baadhi ya shughuli kusimama .
 Naye Meneja wa huduma kwa wateja kutoka kampuni hiyo, Tery Odiko
 alisema kuwa, kampuni hiyo imejiwekea mikakati zaidi ya kuhakikisha
 inafikisha huduma zake katika maeneo ya vijijini ambapo huduma za
 umeme hazijawafikia wananchi.
 Alisema kuwa,huduma hizo wanazotoa zimekuwa zikisaidia kukuza ajira
 kwa vijana kwani kwa kumiliki mitambo hiyo wana uwezo wa kuanzisha
 shughuli mbalimbali za kuwaingia kipato muda wote kama vile salon
 sehemu ya kuchajia simu  kwa kuwa na umeme wa uhakika.
 Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kununua mitambo ya sola kwa
 msimu huu wa sikukuu kwani wanatoa ofa maalumu kwa wateja wake
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment