Daktari ampiga ngumi mgonjwa na kumuua

Kanda ya video ya CCTV imetolewa ambapo daktari mmoja nchini Urusi alimpiga ngumi mgonjwa na kumuua.
Kisa hicho kilitokea katika mji wa Belgorod kilomita 670 kusini mwa mji mkuu wa Moscow mnamo mwezi
Disemba tarehe 29.
Mgonjwa huyo alikuwa amempiga teke muuguzi mmoja kabla ya daktari huyo kumpiga ngumi ya kichwa kulingana na vyombo vya habari vya Urusi na kuzirai kabla ya kuaga dunia akiwa hospitalini.
Wachunguzi wanadhani kwamba hakumuua kwa makusudi lakini wameanzisha kesi ya uhalifu.
Habari hiyo ilisambaa baada ya kanda hiyo kutolewa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment