Mahabusu wawili wa Gereza la Wilaya ya Musoma mkoani Mara, wamefariki dunia baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu
Mkuu wa gereza hilo, Shaku Humba alisema kuwa wafungwa saba na mahabusu watano walioripotiwa kuugua ugonjwa huo.
Hata hivyo hakuwataja majina marehemu hao akisema kuwa hana mamlaka kisheria hadi hapo taratibu zitakapokamilika.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Musoma, Dk Honorata Rutatenisigwa alisema mahabusu
wanaogua ugonjwa huo wamelazwa katika kambi ya gereza hilo.
Dk
Rutatenisigwa alisema usafi katika gereza hilo unaendelea kusimamiwa
kwa karibu, huku unyunyiziaji wa dawa ya kuua wadudu na kutoa huduma ya
kwanza kwa wengine ambao hawajakumbwa na ugonjwa huo ikiendelea.
“Kutokea
kwa vifo hivyo vya mahabusu wawili kumefanya kuwa na jumla ya watu 11
waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mjini Musoma,” alisema.
Wagonjwa hao walifariki kwa nyakati tofauti, baada ya kuugua ugonjwa huo uliolikumba gereza hilo Desemba 29, mwaka jana.
Alisema ugonjwa huo hadi unalikumba gereza hilo uliingia mjini hapa miezi miwili iliyopita.
Dk Rutatenisigwa alisema juhudi za kuudhibiti zinaendelea.
Tayari
ugonjwa huo umeikumba mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, Mwanza ukiongoza kwa
kuathirika zaidi kutokana na idadi ya wagonjwa kuwa zaidi ya 900 katika
wilaya zake zote pamoja na vifo zaidi ya watu 25.
Wilaya za mkoa huo ambazo zimekuwa zikiripoti kuwa wagonjwa mara kwa mara ni Ukerewe, Ilemela, Magu na Nyamagana.
Ili
kukabiliana na ugonjwa huo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, imepiga marufuku uuzaji ovyo wa vyakula.



0 comments :
Post a Comment