Arsenal kwa sasa wanaongoza katika ligi kuu Uingereza
Shabiki mmoja wa Arsenal alifanikiwa kumshawishi mkewe wampe mtoto wao jina la Arsenal bila mwanamke huyo kugundua hilo
.Ilikuwa ni baada ya miaka miwili ambapo mwanamke huyo Clare Smith alijulishwa ujanja ambao mumewe alikuwa ametumia.
Bi Smith, kutoka eneo la Blacktown jimno la New South Wales nchini Australia, alifichua hayo kwenye barua aliyoandikia jarida moja ambapo anasema mwenyewe hakugundua hilo hadi mumewe alipomwambia.
"Tuliamua kumwita binti wetu Lanesra, kwa sababu lilikuwa jina la kipekee na la kupendeza,” aliandika.
Habari kuhusu kisa hicho zimeenezwa sana mtandaoni, wengi wakijaribu kuandika majina ya klabu za Ligi ya Uingereza kutoka nyuma.
Lanesra (Arsenal)
Retseciel (Leicester)
Yticnam (Man City)
Mahnettot (Tottenham)
Detinunam (Man United)
Mahtsew (West Ham)
Looprevil (Liverpool)
Droftaw (Watford)
Ekots (Stoke)
Notreve (Everton)
Aesnaws (Swansea)
Eltsacwen (Newcastle)
Dnalrednus (Sunderland)
Allivnotsa (Aston Villa)
Aeslehc (Chelsea)


0 comments :
Post a Comment