Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akimsikiliza
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala
ya Madini, Profesa James Msofe wakati wa kikao cha utambulisho wa
viongozi wapya Wizarani. Wengine kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara
Profesa Justin Ntalikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia
masuala ya Nishati, Dkt. Eng. Juliana Pallangyo.
………………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, DSM
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Muhongo amewataka Watendaji wa Wizara, Wakuu wa Taasisi
zilizochini yake na watumishi wote kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha
kwamba sekta za Nishati na Madini zinakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa
ikiwemo mabadiliko kiuchumi kupitia sekta hizo.
Profesa Muhongo ameyasema hayo
wakati wa kikao cha utambulisho wa viongozi wapya wa Wizara
kilichoshirikisha Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo chini yake
zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya
Petroli la Tanzania (TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo
cha Madini Dodoma (MRI) na Watendaji kutoka Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC).
“Ni lazima tujitume, hili ndio
jukumu letu la kwanza. Wananchi wanataka umeme na wanataka mabadiliko
kupitia sekta za nishati na madini. Tufanye kazi kwa umoja na uwazi
kwasababu tumepewa fursa ya kuwatumikia wananchi hivyo ni lazima
tubadilike na mabadiliko ni lazima. Asiyeweza kuendana na kasi ya awamu
hii aondoke, hakuna atakayeonewa,” ameongeza Prof. Muhongo.
Prof Muhongo aliongeza kuwa,
kutokana na uzoefu wa viongozi hao na watendaji wa Wizara na Taasisi
anaamini kuwa yatakuwepo mabadiliko katika sekta hizo kutokana na sifa
zao kitaaluma na kiutendaji. “Wananchi wana imani kubwa na uteuzi wetu
na uwepo wetu katika wizara. Tufanye kazi kwa manufaa ya Taifa”,
amesema prof. Muhongo
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara, Profesa Justin Ntalikwa alieleza kuwa, uongozi huo unatarajia
kufanya kazi kwa uadilifu na umakini na kuongeza kuwa, “ jukumu lililo
mbele yetu ni kubwa tunahitaji kufanya kazi kwa bidii tukitumia uzoefu,
wote kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu”,amesema Profesa Ntalikwa.
Naye, Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Madini, Profesa James Msofe, amesema kuwa,
aanatarajia kujifunza kwa kasi kubwa majukumu yake ili kuweza kufikia
matarajio ya wananchi na taifa

0 comments :
Post a Comment