Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage akitoa maelezo Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangala wakati alipotembelea katika hospitali hiyo leo na
kujionea hali halisia ya huduma zinazoendelea katika hospitali hiyo,
Katikati ni Dk Mark Msetti Mkuu wa huduma za Kliniki.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Ocean Road Dk.
Julius Mwaiselage wakati alipotembelea kitengo cha huduma za Bima ya
Afya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Ocean Road Dk.
Julius Mwaiselage wakati alipotembelea kitengo Mionzi , kulia ni
Dk.Hemed Mnyanza Meneja wa Kitengo cha Mionzi.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akitembelea ujenzi wa jengo jipya litakalofungwa mitambo ya miozni
katika Hospitali ya Ocean Road.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akikaribishwa na Mkemia mkuu wa Serikali wakati alipotembelea taasisi
hiyo leo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akipata maelezo kutoka kwa Emmanuel Gwae Mkuu wa Kitengo cha Upimaji
wa Vyakula na Madawa ya Kulevya, kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali
Prof. Samwel Manyele.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akipata maelezo kutoka kwa Emmanuel Gwae Mkuu wa Kitengo cha Upimaji
wa Vyakula na Madawa ya Kulevya, kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali
Prof. Samwel Manyele.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akipata maelezo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele
wakati alipotembelea na kukagua maabara za taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala
akisisitiza jambo wakati alipotembelea na kukagua maabara ya kupima
Vinasaba DNA katika taasisi hiyo, huku Mkemia Mkuu wa Serikali Prof.
Samwel Manyele akimsikiliza kushoto ni Groria Omary Mkuu wa Kitengo
hicho.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Magreth Kinabo- MAELEZO
Serikali imepiga marufuku tabia
ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa
wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo hawakuagizwa kuvipima na
madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya hivyo ni kuiongezea
Serikali gharama zisizo la lazima.
Tamko hilo limetolewa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara ya kutembelea leo kwenye
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dares Salaam.
Waziri Kingwangala alitoa agizo
hilo baada ya kukutana na mgonjwa ambaye alitakiwa kufanya kipimo cha
MRI katika hospitali moja ya binafsi jijini Dar es Salaam, lakini
hospitali hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo vingine ambayo havikupaswa
kupimwa.
Alisema fedha zilizotumika
kulipia vipimo hivyo vya ziada vingetumika kununulia dawa na vifaa tiba
ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Aidha Naibu Waziri huyo
aliwataka watendaji wa afya kutumia utaalamu na ujuzi wao kuaanda
mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto za sekta ya afya nchini.
“Ni lazima tutumia utaalamu
tulioupata katika kupunguza shida za watu katika sekta ya afya. Tumumie
elimu tuliyoipata shuleni na vyuoni ili kuboresha maisha ya Watanzania
na tumsaidie Rais John Pombe Mafuguli tusisubiri hadi tuambiwe tufanye
nini,”alisisitiza.
Mgonjwa huyo ambaye matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kitendo cha hospitali hiyo
kilionesha kumsikitisha Naibu Waziri huyo kwa kuwa fedha za Serikali
ndizo zinazotumika kugharamia vipimo ambavyo, taasisi hiyo
haikumwandikia mgonjwa huyo.
“ Hospitali hii imetumia nafasi
hiyo ya kupima mgonjwa huyo vipimo ambayo hakuandikiwa na daktari
aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza baadhi ya vipimo ambayo
amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii imetumia vibaya mfumo
wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya ziada,alisema Naibu
Waziri Kigwangala.
Aliwataka watendaji wa afya
kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya MRI na
CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa kuwa hospitali
hiyo ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi vizuri kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri huyo aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.
“Sitisheni malipo ya vipimo vya
ziada katika hospitali hiyo, mgonjwa ni wa taasisi hii anaigiliwa na
taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo vingine ambavyo havikupaswa kupimwa,
hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa hapahapa,” alisema Waziri
huyo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri
huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya vipimo
vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani, dawa, ambapo alisema
atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo.Pia
aliutaka uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara
kufanya kazi kama timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.


0 comments :
Post a Comment