Ligi Daraja la Daraja la Kwanza
(StarTimes League) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa
michezo kumi
na mbili kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kituo cha
StarTv kikitarajiwa kuonyesha moja kwa moja michezo miwili ya ligi hiyo.
Kundi
A Ijumaa, Januari Mosi 2016 Polisi Dar watawakaribisha Mji Mkuu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku kesho Jumamosi michezo tisa ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
A Ijumaa, Januari Mosi 2016 Polisi Dar watawakaribisha Mji Mkuu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku kesho Jumamosi michezo tisa ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Jumamosi StarTv watakua uwanja wa
Karume jijini Dar es salaam kurusha moja kwa moja mchezo kati ya
Ashanti United dhidi ya Polisi Dodoma, Polisi Morogoro watawakaribisha
Kurugenzi FC ya Mafinga katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku
Kimondo FC wakicheza dhidi ya Burkinafaso kwenye uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya.
Maafande wa Ruvu Shooting
watacheza dhidi ya Mji Njombe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli
dhidi ya JKT Mlale katika uwanja wa Wambie mkoani Iringa, maafande wa
JKT Kanembwa wakiwakaribisha Mbao FC katika uwanja wa Lake Tanganyika
mjini Kigoma.
Geita Gold watawakaribisha Polisi
Mara kwenye uwanja wa shule ya Nyankumbu mjini Geita, JKT Oljoro
watacheza dhidi ya Rhino Rangers uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha, huku maafande wa Polisi Tabora wakiwakaribisha Panone FC katika
uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
StarTv Jumapili wataonyesha moja
kwa moja mchezo kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United uwanja wa
Karume, huku timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) wakicheza dhidi
ya Friends Rangers katika uwanja wa Mlandizi Mabatini.


0 comments :
Post a Comment