==>Watuhumiwa Sugu Wa Dawa Za Kulevya Kufikishwa Mahakamani
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa
tuhuma za kujihusisha na mtandao wa kuuza madawa ya kulevya hapa
nchini.
Watuhumiwa hawa ni miongoni mwa wauza madawa wazoefu na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka yanayowakabili.
Watuhumiwa
hao walikamatwa na kilogram 09 za madawa ya kulevya aina ya HEROINE
kutoka nchini Pakistan mwaka 2015 ni kama ifuatavyo:
1.MOHAMED
S/O ABDALLA OMARI, Miaka 37, mfanyabiashara, mkazi wa Tegeta Nyuki,
anatuhumiwa kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya na usafirishaji
haramu wa binadamu. Anatuhumiwa kumsafirisha MWINYI S/O MGOBANYA, Mkazi
wa Ununio na kumweka rehani (bond) huko Pakistan kisha akachukua madawa
ya kulevya kwa mali kauli.
2.NASSORO
S/O SULEIMAN, Miaka 35, meneja wa TUNGWE BUREAU DE CHANGE katika jengo
la IPS jijini Dar es Salaam anatuhumiwa kwa kosa la kushirikiana na
genge la wauzaji wa madawa ya kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha
pesa kwa njia ambazo sio rasmi.
Mtuhumiwa
wingine DAUD S/O AYUBU ADAM @ KANYAU, Miaka 46, Mfanyabiashara mkazi wa
Salasala jiji Dar es Salaam na Kibaha. Anatuhumiwa kusafirisha madawa
ya kulevya lakini hatafikishwa mahakamani kwa kuwa uchunguzi dhidi yake
bado unaendelea.
Takwimu
zinaonyesha kuwa Mwaka 2014 kiasi cha kilogram 304.61 za HEROINE na
kilogram 29.68 za COCAINE kilikamatwa na watuhumiwa 14501 ambapo
miongoni mwao watanzania walikuwa 14467 ikilinganishwa na mwaka 2010
ambapo zilikamatwa kilogram 123 za HEROINE na kilogram 16.74 za COCAINE
na watuhumiwa 23 walikamatwa watanzania wakiwa 22
Uchunguzi
umebaini kuwa sababu kuu ya ongezeko la takwimu hizi ni kushamiri kwa
mitandao ya wahalifu wa kimataifa wa madawa ya kulevya wanaoshirikiana
na watanzania kufanya biashara ya kusafirisha binadamu kwenda nchi
wazalishaji wa madawa ya kulevya katika nchi za kiarabu na kuwaweka
rehani ili wapatiwe kiasi kikubwa cha madawa kwa mali kauli.
Hatima
ya watanzania wanaowekwa rehani ni kupigwa mijeredi kwa nyaya za umeme,
na wakati mwingine kuuawa ili hali wale waliowapeleka huko huendelea
kujineemesha.
Kutokana
na tathmini hiyo, Jeshi la Polisi tumeanzisha mikakati inayolenga
kusambaratisha mitandao ya magenge ya uhalifu yanayofanya uhalifu hapa
nchini na nje ya nchi za nje ili kupunguza au kuzuia uingizwaji wa
madawa ya kulevya.
==>Kupatikana Kwa Silaha Inayomilikiwa Kihalali.
Tarehe
09/01/2016 jeshi la polisi liliwakamatwa watuhumiwa wawili JACKSON S/O
JUMANNE, miaka 18, mfanyakazi wa ndani, mkazi wa Bunju “A”, na
DEOGRATIAS S/O PAMBO kwa tuhuma za kuiba silaha Bastola aina ya COMPAQ
CZ75D yenye namba TZCAR 100416 iliyotengenezwa Jamhuri ya CZECH.
Hii
ni baada ya mlalamikaji SAMWELI S/O SAMWANG’OMBI, Mkazi wa Bunju,
Kinondoni jijini Dar es Salaam kutoa taarifa polisi kwamba ameibiwa
silaha hiyo.
Watuhumiwa walipohojiwa walikiri kuiba silaha hiyo na kueleza walipoifisha huko maeneo ya Mtoni kwa Azizi Ally.
Ufuatiliaji
uliendelea ndipo alipokamatwa mtuhumiwa mwingine kwa jina la JOHN S/O
SAMSON MZEZE, miaka 24, mfanyabiashara, mkazi wa kambi ya polisi kilwa
road. ambaye alieleza kuwa siku ya tukio kuna kijana alifika katika eneo
lake la biashara huko mtoni kwa Azizi Ally na kununua soda.
Baadaye
kijana huyo alimtishia JOHN SAMSON MZEZE kwa bastola ili atoe fedha
lakini alipambana nae kwa kushirikiana na wananchi ndipo mhalifu huyo
alipotelekeza silaha hiyo na kukimbia.
JOHN SAMSON MZEZE na wenzake waliisalimisha silaha hiyo kityuo cha polisi Kilwa road
==>Wahalifu Sugu 06 Wa Unyang’anyi Wa Kutumia Silaha Wakamatwa
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 06 kwa tuhuma
za kujihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo
mbalimbali ya jiji na mikoa ya jirani.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa tarehe 11/01/2016 na 16/01/2016 katika maeneo tofauti
kufuatia taarifa za raia wema ambao ni wazalendo kwa nchi yao.
Watuhumiwa
hawa wamehojiwa na kukiri kuhusika katika baadhi ya matukio ya uporaji
wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na kwamba baadhi ya wenzao
wamefungwa gerezani kutumikia adhabu kwa makosa kama haya. Watuhumiwa
hao ni kama ifuatavyo:
1. AGASESE S/O MALA, Miaka 40, Mkazi wa Mbagala Chamazi
2. ABDALLAH S/O JUMA, Miaka 32, Mkazi wa Tandika.
3. KRISTAN S/O NYONI, Miaka 28, Mkazi wa Mbagala Charambe.
4. VICTOR S/O GABRIEL, Miaka ? Mkazi wa Gongolamboto
5. PROSPER S/O GERVAS KALALA @ CHIEF, Miaka 41, Mkazi wa Yombo Kipera
6. MOHAMED S/O ABDUL @ MUD, Miaka 23, Mkazi wa Yombo Buza.
Upelelezi
juu ya watuhumiwa hawa unaendelea na utakapokamilika jalada la kesi
litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali kwa hatua zake muhimu.
==>Kukamatwa Kwa Magari Ya Wizi Pamoja Na Watuhumiwa
Katika
hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa
kukamata magari yaliyokuwa yameibwa maeneo tofauti ya jiji la Dar es
Salaam na mikoani pamoja na watuhumiwa.
1.
Gari na. T271 DCT, Toyota IST, rangi nyeusi imekamatwa huko Mbeya
akiwanayo mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari anayeitwa ROBINSON S/O
SAMWELI, Mkazi wa Mwanjelwa na Sai mkoani Mbeya. Gari hili lilibiwa
nyumbani kwa Dr.REGINARD huko Kimara, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
2.
Gari na. T916 DCL, aina ya Mitsubishi FUSO ambalo liliibwa maeneo ya
Kimara na kukamatwa huko Tegeta Masaiti nyumbani kwa HASSAN S/O PHILIPO
MAZWAZWA ambaye ni mwizi sugu wa magari ambaye anatafutwa. Gari hilo
lilikuwa limebadilishwa baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na kupigwa rangi
nyingine
3. Gari na. T593 CEL, aina ya Toyota Prado iliibiwa huko Regency Estate
4. T.999 DDB, aina ya Toyota Prado, iliyoibwa katika maegesho ya Regency Estate ilikamatwa huko Gezaulole nyumbani kwa mtu.
==>Taarifa Za Usalama Barabarani Kanda Maalum
Katika
hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda
Maalum ya Dar es Salaam kimeendelea kufanya oparesheni ilianza tarehe
02/01/2016 hadi sasa ili kuhakikisha madereva wote wa vyombo vya moto
wanazingatia na kufuata sheria za usalama barabarani muda wote.
Oparesheni
hiyo ililenga kutoa elimu kwa madereva na kuwakamata wale wanakaidi
maelekezo yanayotolewa juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani na
sheria za usalama barabarani.
Pia
magari, pikipiki, na bajaji vilikaguliwa kujua uhalali wake wa kuwa
barabarani. Makosa yaliyokamatwa ni pamoja na matumizi mabaya ya
barabara, ulevi, kukatisha route, kutotii amri, ubovu wa magari na
makosa mengineyo.
Katika
oparesheni hiyo jumla ya magari na pikipiki zilizokamatwa ni 24,068 na
kutozwa faini ya jumla TSHS 722,040,000/= (Millioni mia saba ishirini na
mbili, arobaini elfu tu).
Aidha,
lengo ya Jeshi la Polisi si kukusanya kiasi kikubwa cha fedha bali
kuona watanzania wanazingatia na kutii sheria za usalama barabarani
wakati wote wanapokuwa na vyombo vya moto.
S. N. SIRRO - DCP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


0 comments :
Post a Comment