Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (katikati) akiongoza sala
ya kufungua mkutano wa kwanza baada ya uchaguzi wa kumchagua Meya na
Naibu Meya wa manispaa hiyo.
******Hatimaye baada ya danadana za muda mrefu, uchaguzi wa kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja wa Vyama vinavyunda Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanikiwa kuongoza Manispaa hizo.
Chaguzi
hizo zilizhairishwa mara mbili kutokana na mvutano uliotokewa katika
chaguzi za nyuma, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa amri za mahakama.
Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa hiyo baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepata kura 20. Naibu Meya ni Diwani wa Tandale kwa tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.
Uchaguzi
wa Manispaa ya Ilala leo pia uliingia katika mgogoro kati ya madiwani
wa CCM na wale wa Ukawa, hali iliyosababisha CCM kususia uchaguzi huo na
kuwaacha Ukawa kupiga kura peke yao na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
kumtangaza Charles Kuyeko (Chadema) kuwa mshindi wa kiti cha Meya wa Ilala kwa ushindi wa kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) ambaye amepata kura 31.
Jumla
ya madiwani waliotakiwa kupiga kura katika uchaguzi huo ni 54, hivyo
madiwani 31 wa Ukawa waliobaki ndani walitimiza akidi ya uchaguzi huo
kuendelea.



0 comments :
Post a Comment