Na Woinde Shizza,Arusha
Msafara
wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli uliokuwa ukielekea Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mapema leo umesimamishwa na wananchi
katika eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha ili kushinikiza
kutatua kero zao na changamoto zao ikiwemo kuwepo na kiwanda cha
mafuta ya kupikia cha Mount Meru Mill kinachodaiwa kuchafua
mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Wananchi
hao ambao walijikusanya kuanzia mida ya saa mbili kamili asubui mbali
na kumueleza Rais huyo kero zao, pia walitumia nafasi hiyo kumpongeza
kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu yaliyopo humu
nchini.
Akiongea
mbele ya Rais mara baada ya kupewa nafasi , mmoja wa wanachi wa eneo
hilo la mbauda Thabiti Abubakari alimuomba rais awasaidie kutatua
tatizo la kiwanda hicho kutiririsha maji machafu ya kiwandani kwani
tatizo hilo ni baya na linawaharibia mazingira na kuhatarisha afya zao.
‘’Musheshimiwa
Rais tunapenda utusaidie hapa kwetu mbauda tuna kero kubwa inatusumbua,
kuna hiki kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mount meru mill kimekuwa
kinatiririsha maji machafu ya kiwandani huku nje ambapo wananchi
wanaishi , kiwanda hiki hakijajenga mitaro ya kupitisha maji machafu
hivyo maji yote machafu yakitoka huko kiwandani yanaingia huku majumbani
kwetu, hivyo muheshimiwa tunaomba utusaidie hili tatizo kwani kiwanda
hiki kipo ndani ya makazi ya watu,kinahatarisha afya sasa
inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao wanacheza uku
mitaani pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama kipindupindu maana
maji haya ni machafu sana”alisema Dhabiti
Akijibu
swala hilo Rais magufuli alisema kuwa amelisikia na aliwaagiza mamlaka
ya usafi wa mazingira NEMC kulifuatilia swala hili mara moja .
Aidha
Rais Magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa jiji la Arusha
kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwaahidi kuwa
ataendelea kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa
akifanya kampeni.
Alisema kuwa kipindi hiki hakuja Arusha kwa ajili ya kuongea na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi Arusha kufanya mkutano mkubwa ambao pia atatumia muda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji la hilo.
Alisema kuwa kipindi hiki hakuja Arusha kwa ajili ya kuongea na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi Arusha kufanya mkutano mkubwa ambao pia atatumia muda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji la hilo.
0 comments :
Post a Comment