Viongozi wa nchi kadhaa za Kiafrika wameunga mkono pendekezo la kujiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Mapema jana Jumatatu kwenye sherehe za kufunga kikao cha siku mbili cha viongozi wa nchi za Kiafrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, Rais Idriss Déby wa Chad ambaye hivi karibuni alichukua uenyeketi wa umoja huo, amekosoa mienendo ya mahakama hiyo ya ICC kwa kile alichosema kuwa ni kuwaandama tu viongozi wa Afrika na kusema kuwa, katika nukta zote za dunia hususan nchi za Kimagharibi kumekuwa kukishuhudiwa jinai mbalimbali za
ukiukaji wa haki za binadamu, hata hivyo mahakama hiyo imekuwa ikifumbia macho jinai hizo. Rais Déby ameongeza kuwa, badala ya ICC kutekeleza haki kwa nchi zote bila ya ubaguzi, imekuwa ikielekeza macho yake kwa viongozi wa Kiafrika peke yao.(VICTOR)
ukiukaji wa haki za binadamu, hata hivyo mahakama hiyo imekuwa ikifumbia macho jinai hizo. Rais Déby ameongeza kuwa, badala ya ICC kutekeleza haki kwa nchi zote bila ya ubaguzi, imekuwa ikielekeza macho yake kwa viongozi wa Kiafrika peke yao.(VICTOR)
Viongozi kadhaa wa Kiafrika wameunga mkono kauli ya mwenyekiti huyo mpya wa AU na kuonyesha kuwepo uwezekano wa kujiondoa nchi kadhaa za Kiafrika kwenye mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi.
Kabla ya hapo pia Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, sanjari na kutishia kujitoa nchi yake kwenye mahakama hiyo, alizitaka nchi nyingine za Kiafrika kusitisha uanachama wao ICC kutokana na upendeleo wake.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliayonzisha shughuli zake mwaka 2002 kwa lengo la kuwahukumu watenda jinai za kivita ambao bado walikuwa hawajashtakiwa, hadi sasa imezifanyia kazi kesi nane yaani Kenya, Côte d’Ivoire, Libya, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda na Mali.CHANZO:IRANSWAHILI


0 comments :
Post a Comment