TED CRUZ AMSHINDA TRUMP MCHUJO WA IOWA


    TrumpSeneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.
Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya
Wabunge Uingereza wamjadili Trump Trump asema Cruz hafai kuwa rais Marekani Palin amuunga mkono Donald Trump
Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.
Image copyright Getty Image caption Bw Trump amempongeza Bw Cruz Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika kumaliza katika nambari mbili.
Wagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi.
Utaratibu wa kuchagua wagombea Marekani
Duru za karibu na mgombea wa Democratic Martin O'Malley, aliyekuwa gavana Maryland, zimeambia BBC kwamba atasitisha kampeni yake, na kufanya ushindani mkali sasa kuwa kati ya wagombea wawili.
Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.CHANZO:BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment