Ligi Kuu ya Hispani (La Liga) iliendelea hapo jana kwa michezo kadhaa mchezo mkubwa ukiwa ni Real Mdrid iliyokuwa mwenyeji wa Atletico katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mchezo huo ulimalizika kwa Atletico kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli lililofungwa na Antoine Griezmann katika dakika ya 53 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Filipe Luis.
Baada ya matokeo hayo Atletico imefikisha alama 58 na kusalia katika nafasi ya pili nyuma ya Barcelona iliyofikisha alama 63 huku Real Madrid ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 54.
Matokeo ya michezo mingine;
Getafe 0 – 1 Celta Vigo
Sporting Gijon 2 – 4 Espanyol
Real Betis 2 – 2 Rayo Vallecano