Nkupamah media:
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa chama hicho Omar Said Shaban baada
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kulalamika kimeshangazwa na kitendo cha
Maalim Seif kuendelea kubaki mitaani tangu kujitangazia mshindi wa urais
wa Zanzibar wakati ni kinyume na sheria ambayo inakataza na kaunishwa
wazi hatua zinazopaswa kuchuliwa.
Akizungumza na Nipashe mjini Zanzibar jana, Omar alisema kuwa, kazi
ya kufungua mashitaka na kutetea kesi mahakamni ni jukumu la Mkurugenzi
wa Mashitaka kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Alisema kama Maalim Seif kupitia CUF alifanya kosa la jinai
kujitangaza mshindi kabla ya Tume ya Uchaguzi (ZEC) kufanya hivyo, DPP
ndiyo anaweza kusema kama kuna kesi ya kujibu au hakuna na sio
wanasiasa.
“Mkurugenziwa mashitaka aachiwe afanye kazi yake bila ya kuingiliwa
na wanasiasa, kama kuna kesi ya kujibu au la ushahidi na vielelezo
vitasema,”alisema Omar.
Hata hivyo alisema kuwa suala la Maalim Seif kukamatwa na
kufunguliwa mashitaka limekua na utata mkubwa kutokana na Naibu
Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi, kueleza
jalada la uchunguzi kuhusiana na sula hilo limekamilika na kukabidhiwa
DPP, wakati CUF kinadai Maalim Seif hajawahi kukamatwa na kuhojiwa na
polisi tangu kujitangaza mshindi Oktoba 26, mwaka jana kabla ya kufutwa
kwa matokeo ya uchaguzi huo.
Omar alisema kwa mujibu wa taratibu za uchunguzi, haiwezekani
kufungua jalada la uchunguzi kabla ya kumuhoji mtuhumiwa na kumchukua
maelezo kama kielelezo cha ushahidi wa mashitaka dhidi yake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments :
Post a Comment