TFF YAONYA UPANGAJI WA MATOKEO

Nkupamah Media:

gsShirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi za ngazi
mbalimbali za nchini.
TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.
Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali zitachukuliwa .
TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment