Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Christopher Ngubiagai
amewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana watumishi sita wa idara ya
afya akiwemo Maimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Timoth Sumbe, kwa tuhuma ya
ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 145 za mfuko wa afya ya jamii
(CHF).
Wengine
waliosimamishwa kazi ni aliyekuwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Iramba, Dk. Japhet Simeo ambaye kwa sasa amehamia Tandahimba.
Pia
wamesimamishwa kazi Katibu wa Afya Wilaya ya Iramba, Kalebi Ngughu,
Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Sylveri Maganza, Katibu wa afya
Alphonce na Katibu mwingine wa afya, Grace Maganga.
Akitoa
tamko hilo zito mbele ya kamati ya ulinzi ya wilaya ya Iramba na
waandishi wa habari, Ngubiagai alisema ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba, Halima Mpita ambaye amehamishiwa
Tunduma akamatwe na kuletwa Iramba, ili kujibu tuhuma ya ubadhirifu huo
wa fedha za umma.
“Nimewasimamisha
kazi wafanyakazi hawa, ili kupisha uchunguzi wa kina uweze kufanyika na
ikithibitika wanahusika na upotevu huo wa fedha CHF na `on call
allowance` hatua za ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma zichukue
sehemu yake,” alisisitiza.
Akifafanua,
Ngubigai ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, alisema kati ya fedha
hizo, shilingi milioni 64 ni gawio lililotolewa na mfuko wa taifa wa
bima ya afya (NHIF) kutokana na ada zilizolipwa na wanachama wa CHF
wilaya ya Mkalama.
“NHIF
ilitos fedha hizo Julai mosi, 2013 kipindi wilaya ya Iramba
ilijumuisha na jimbo la Iramba mashariki kwa wakati huo ambalo lilipata
hadhi na kuwa wilaya ya Mkalama na uchunguzi wa awali unaonyesha fedha
hizo hazikuingizwa kwenye akaunti yoyote zimeishia hewani,” alisema DC
huyo kwa masikitiko.
Kaimu
mkuu wa wilaya ya Iramba na mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoani
Singida,akitoa taarifa ya kusimamisha watumishi wa idara ya afya kwa
tuhuma ya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi 145 milioni za mfuko wa afya
ya jamii (CHF) na za posho za watumishi wa afya (on call allowance),kwa
waandishi wa habari (hawapo kwenye picha),Pia ilikuwepo kamati ulinzi na
usalama ya wilaya ya Iramba. (Picha na Nathaniel Limu.)
Aidha,
alisema shilingi 81,180,000 za ‘on call alowance’, nazo hazikulipwa kwa
walengwa na badala yake zimetumika kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Kaimu
mkuu huyo ya wilaya alisema kuwa halmashauri ya Mkalama inafanya kazi
ya ziada kudai fedha hizo kwa barua kumbukumbu MDC/A.10/3/27 ya
14/4/2014, MDC/ A.10/3/7 YA Julai 15/ 2014 na MDC/A.10/3/8 ya
15/2/2016, zote hazikuzaa matunda na hazijajibiwa hadi sasa.
“Kuna
kila dalili kwamba wapo viongozi wa ngazi za juu ambao wameongoza kwa
nyakati tofauti wameshiriki katika ‘dili’ hili chafu la kutumia fedha za
umma kwa maslahi yao binafsi,hatutawaacha,tutawafuata huko waliko
kuwakamata,ili kuja kujibu tuhuma hii,” alisema.
Ngubiagai
ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa umma wa wilaya ya Iramba na
Mkalama kwenda sambamba na mapinduzi ya sasa ya kiutendaji ya “Hapa
kazi tu”, na kuacha vitendo vya ubarudhilifu wa mali ya Umma ikiwemo
rasilimali fedha kwa madai vitawaharibia maisha yao.
0 comments :
Post a Comment