Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliendelea hapo jana kwa michezo sita ambapo Leicester City iliendelea kukwea kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Norwich City.
Goli pekee la Leicester City lilifungwa na Leonardo Ulloa katika dakika ya 88 na hivyo kuiwezesha Leicester City kufikisha alama 56 ikiwa mbele kwa alama tano kwa timu inayoshika nafasi ya pili, Tottenham Hotspur.
Mchezo mwingine ulikuwa ni Chelsea iliyowafata Southampton na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja, magoli ya Chelsea yakifungwa na Fabregas dakika ya 75 na  Branislav Ivanovic dakika ya 89 na goli la Southampton likifungwa na Shane Long katika dakika ya 42.
Matokeo mengine ni;
West Ham United 1 – 0 Sunderland
Leicester City 1 – 0 Norwich City
Stoke City 2 – 1 Aston Villa
Watford 0 – 0 Bournemouth
West Bromwich 3 – 2 Crystal Palace
Ligi hiyo inataraji kuendelea leo kwa michezo miwili,
Manchester United – Arsenal        17:05 EAT
Tottenham – Swansea City            17:05 EAT