Nkupamah media:
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na
wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za
Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8
walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka
nchini Kenya.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye
riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
Mshindi
wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama
ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisoma risala
mara baada ya kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo
aliwapongeza wahiriki wote, wadhamini na kuwataka Watanzania kutumia
mbio hizo kama fursa ya kuutangaza utalii uliopo nchini.
0 comments :
Post a Comment