Mmiliki wa klabu wa Chelsea, Roman Abramovich ameudhibitishia uongozi wa Chelsea na wachezaji wa klabu hiyo kuwa kocha Antonie Conte ndiyo ataiongoza klabu hiyo baada ya msimu huu kumalizka.
Mtandao wa Express Sport umeripoti kuwa Conte alikutana na Abramovich kuzungumza kuhusu dili hilo la kuiongoza Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu ukiwa na thamani ya Pauni Miloni 18.
Hatua hiyo ya kumchukua Conte kuwa kocha wa Chelsea limekuja baada ya kocha huyo wa Italia kutangaza kuachana na kazi ya kuiongoza Italia baada ya kumalizika kwa mashindano ya Euro 2016 ambayo yatafanyika Ufaransa mwezi Juni na Julai mwaka huu.



0 comments :
Post a Comment