Kitengo
cha mizigo cha Etihad kimepokea ndege mpya aina ya Boeing 777 ambayo
itawezesha kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad kundelea
kutanua mipango yake kwa mwaka 2016. Ndege hiyo imekua ya 11 katika
kitengo hicho ambapo tayari imeshaanza kazi rasmi Machi, 1 mwaka huu.
Kitengo
cha mizigo cha Etihad kilitangaza kuwa kingepokea ndege zingine mbili
katika maonyesho ya ndege ya Dubai mwaka jana, na kutumia sehemu ya Dola
Bilioni 67 za kimarekani kwa oda iliyotolewa mwaka 2013 kwa ajili ya
ndege 199. Ndege hizo mbili zilizoongezwa zina thamani ya Dola Milioni
637 za kimarekeni na ndege ya pili imewasili Abu Dhabi mwezi huu.
Ndege
hizo mpya zitakua na siti tisa ambazo zitaruhusu kitengo hicho cha
mizigo cha Etihad kubeba na watu wengine kama sehemu ya mpango wa kubeba
farasi wasafirishwao kwa anga, ambayo inasaidia kwa wanyama hao wenye
thamani kubwa. Zitakua ndege za kwanza katika kitengo cha mizigo cha
Etihad kuwa katika muundo huu. Wanyama wasafirishwao kwa anga husimamiwa
na mameneja ambao pia husaidiwa na timu ya watunzaji wakiwa angani na
pia ardhini, ambapo farasi hao watasafirishwa kwenda sehemu tofauti
katika mabara ya Ulaya, Asia, Amerika, Afrika na Australia.
Kevin
Knight, Afisa Mkuu wa mipango na mikakati wa shirika la ndege la Etihad
alisema, “Ndege iliyoongezwa inatupa fursa ya kutanua kitengo chetu cha
mizigo na kukuza soko letu pia. Mwaka uliopita, tuliweza kujitanua
katika mabara ya Amerika ya Kusini, Afrika na Asia na ndege hii mpya
itaongeza uwezo na kutuwezesha kukua zaidi kwa kupitia mtandao wetu,
lakini la muhimu ni pia kuongeza fursa za kukuza mikataba yetu sehemu
mbali mbali duniani”
Mwaka
2015, kitengo cha mizigo cha Etihad kilikuza upatikanaji wake
ulimwenguni kwa kutoa huduma katika vituo vipya 6 vya shirika la ndege
la Etihad ikiwa ni pamoja na Edinburgh, Madrid na Kolkatta. Etihad sasa
inafanya kazi za huduma ya mizigo kwa ratiba maalum katika vituo vya
mizigo pekee ambavyo ni; Hahn, San Juan, Bogota, Guangzhou, Dakar,
Douala, Eldoret, Hanoi, Houston, Nouakchott, Sharjah na Tbilisi.
Ndege
zilizopo kitengo cha mizigo cha Etihad kwa sasa zipo tatu aina ya
Boeing 777Fs, Boeing 747s na Airbus A330s. Kitengo hicho cha mizigo cha
nchi za umoja wa Kiarabu kwa sasa kinahudumia vituo 14 vya mizigo pekee
duniani kote kutoka katika kituo chake kikuu cha Abu Dhabi na ina uwezo
wa kubebwa juu ya meli ya shirika la ndege la Etihad yenye uwezo wa
kubeba abiria zaidi ya 100.
“Toka
iingie katika huduma miaka 7 iliyopita, ndege ya mizigo 777 imezidi
kutambulika kama ndege bora ya mizigo kubwa na bora duniani yenye injini
mbili pacha,” alisema Marty Bentrott
Makamu
wa Rais wa Mauzo Etihad kwa Mashariki ya Mbali, Urusi, na Asia ya kati.
“Tunajivunia kuwa na ndege ya mizigo 777 ikiwa na mchango muhimu katika
kitengo cha mizigo cha Etihad wakati ikiendelea kuimarisha na kukuza
kitengo hicho sehemu mbali mbali duniani”.
Kitengo
hicho cha mizigo cha Etihad huingiza zaidi ya dola bilioni moja kama
mapato yake kwa mwaka na kuripotiwa kukua kwa kasi kubwa kwa mwaka 2015
kikiwa na tani 592,090 za mizigo na barua pepe zilizosafirishwa kwa
ujumla, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 toka hesabu za mwaka
2014. Kitengo hicho pia ndicho kiini kwa asilimia 88 kwa kuingiza na
kusafirisha mizigo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.
Kikiwa
kimeanzishwa mwaka 2004, kitengo cha mizigo cha Eihad ndicho kitengo
kikuacho kwa kasi katika kampuni ya ndege ya Etihad. Toka katika kituo
chake kikuu kilichopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi, kitengo
cha mizigo cha Etihad kinatoa huduma mbali mbali za mizigo kwa wateja
wake kikihusisha na ukuaji wake kimataifa.


0 comments :
Post a Comment