Miongoni
mwa mambo ambayo yanachangia vijana wengi kukaa vijiweni na hata
kujiingiza katika makundi mabaya ni pamoja na uvivu. Ili kuendana na
kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ wadau wa masuala ya Kilimo hapa nchini,
KolimoJoint wao wamekuja na mkakati kabambe wa kuwainua vijana katika
kufikia malengo yao hasa katika suala la kilimo.
“Hapa Kazi Tu’, Ni kauli mbiu aliyokuja nayo mheshimiwa rais wa awamu ya tano Tanzania Dk. John Magufuli Pombe ambayo nasi kama #KilimoJoint tunapenda
kuituma ili mkulima mdogo hususani kijana aweze kujikwamua katika
maisha kwa kujiajiri kwa kupitia kilimo na ufugaji” wanaelezea
KilimoJoint.
Miongoni mwa huduma wanazotoa ni pamoja na ushauri na usambazaji wa-Umwagiliaji
wa njia ya matone, Mbegu, kitalu nyumba, Mafunzo na ufuatiliaji,Insect
nets,Solaring covers, Ufugaji wa samaki, Kapeti za kuhifadhia
maji,Chakula cha samaki na mambo mbalimbali yanayohusu Kilimo.
Ilikumsaidia kijana kufikia malengo yake, pia waweza kuwasiliana n KilimoJoint kupitia barua pepe kilimojoint@gmail.com au kupitia kurasa yao ya mtandao wa kijamii wa facebook.
“Kilimo cha kisasa sio uchafu”.


0 comments :
Post a Comment