Timu
ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge
Sports Club usiku wa leo Aprili 26.2016 imeweza kutoka sare ya bao 1-1,
dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Unguja na kushuhudiwa na
watu mbalimbali.
Mchezo
huo wa aina yake na wa kipekee kwa kikosi hicho cha Bunge Sports Club
kiliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia wakati wote ambapo
waliweza kupata bao lao la kuongoza ndani ya dakika 22 ya mchezo katika
kipindi cha kwanza bao safi lililofungwa kwa kushuti la nje ya 18 na
kuwaacha Wachezaji wa Baraza la Wawakilishi wasijue la kufanya.
Bao
hilo la Bunge Sports Club ambalo lilikuwa la ushindi lilidumu hadi
kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 67, Timu ya Baraza la
Wawakilishi ilifanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo kuwa 1-1.
Bao hilo lilipachikwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hasa mvua
kiasi cha kuwapoteza vibaya wachezaji wa timu ya Bunge ambao walicheza
katika mazingira magumu sana.
Mara
baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge
Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamoto alibainisha kuwa
kikosi chake kilicheza soka safi na wataendelea kukiimalisha kwani
wanaamini mpira ni ajira ambapo pia alieleza kuwa bila washindani wao
‘kuwachomekea’ wanahakika wangefanya vizuri zaidi n ahata kuibuka na
mabao mengi.
Kwa
upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid
alizipongeza timu zote mbili na kuzitaka kuendelea kudumisha michezo na
suala la Muungano kwa ujumla kwani wanahakika kupitia michezo suala hilo
litaenziwa kwa miaka yote.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh.
January Makamba alibainisha kuwa wataendelea kuulinda Muungano huku
akiwataka Watanzania kuishi kwa misingi ya Amani na utulivu kwa kipindi
chote ambapo pia alieleza kuwa suala la Michezo litaendelea kuwapo
ilikuongeza mshikamano kwa watu wote.


0 comments :
Post a Comment