Manchester City ipo njia panda kukosa huduma ya kiungo mchezeshaji wa klabu hiyo, David Silva katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA dhidi ya Real Madrid baada ya jana kutoa kupata majereha.
Silva alitoka kipindi cha kwanza katika mchezo wa jana Jumanne dhidi ya Real Madrid baada ya kupata majeraha ya misuli na kocha wake, Manuel Pellegrini kusema kuwa hana uhakika kama Jumatano ya wiki ijayo atakuwa amepona.
“David alikuwa mzito kidogo, ni ngumu kusema kwa sasa lakini ni ngumu kwake kupona ndani ya wiki moja,” alisema Pellegrini.