Daktari
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara akiwaongoza
wabunge kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na madaktari na wauguzi wa
idara hiyo Leo.
Dk.
Upendo Ndara wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali akiwaeleza
wabunge wa Kamati ya Afya jinsi idara hiyo inavyowahudumia wagonjwa wa
dharura na ajali wanaofikishwa hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis
Kigwangallah akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ambayo imeitembelea
leo hospitali hiyo.
Dk
Upendo Ndara wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali akiewaeleza
wabunge wa Kamati ya Afya juu ya upanuzi wa jengo la kuwahudumia
wagonjwa wa dharura na ajali kwenye hospitali hiyo.
Mkuu
wa Idara ya Wagonjwa wa Afya Akili, Dk Frank Massawe akiwaeleza wabunge
wa Kamati ya Afya jinsi idara hiyo inavyotoa tiba kwa wagonjwa wa
akili.
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa, Lawrence Museru
akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Afya kuhusu huduma zinazotolewa
kwa wagonjwa wa akili.
Mkuu
wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (mwenye koti) akiwaeleza wabunge
wa Kamati ya Afya jinsi mashine ya CT- SCAN inavyochukua vipimo
mbalimbali kwa wagonjwa. Dk Lwakatare amewaeleza wabunge hao kwamba
mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kugundua matatizo ya wagonjwa.
Na John Stephen
Kamati
ya Afya ya Bunge leo imeitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
kwa ajili ya kukagua huduma mbalimbali za afya zinazotolewa na
hospitali hiyo.
Ziara
hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Joseph Serukamba
akiwamo Mussa Azzan Zungu na wabunge wengine wa kamati hiyo.
Wabunge
hao wametembelea Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Idara ya
Magonjwa ya Akili, Idara ya Mionzi na Wodi ya Mwaisela na chumba cha
kuchakacha gesi ambayo inatumika wakati wa kutoa tiba kwa wagonjwa
mbalimbali.
Daktari
wa magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara amewaeleza wabunge hao
jinsi madaktari na wauguzi wanavyowahudumia wagonjwa wanaofikishwa
kwenye idara hiyo, changamoto na jinsi wanavyofanikiwa kuokoa maisha ya
wagonjwa wa ajali na wagonjwa wengine.
Pia,
Dk Upendo ameelezea juhudi kubwa zinazofanywa na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) katika kupanua jengo la idara hiyo ili kutoa huduma bora
za matibabu kwa wagonjwa.
Naye
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza
wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa
matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
0 comments :
Post a Comment