Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (aliyesimama) akizungumza na wadau
wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati
wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau hao jana Jijini Mwanza
pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na
kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini
hapo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na
kulia ni katibu wa CCM Mwanza Ndg. Miraji Mtaturu
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (wapili kulia) akizungumza na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye
alipowasili ofisini kwake wakati wa ziara yake jana Jijini Mwanza
kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi
kwa maafisa habari wa mkoa na kutembelea viwanja vya Michezo na vituo
vya utangazaji vilivyopo Jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Mwanza Bw. Ndaro Kulwijira.
Afisa
Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Ndg. Atley Kuni akitoa taarifa ya
sekta ya habari kwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye
kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana
Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa
huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo
jijini hapo.
Msanii
kutoka jiji la Mwanza Ndg. Feizal Saul (aliyesimama) akichangia wakati
wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Nnauye kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa
vitendea kazi kwa maafisa habari na kutembelea viwanja vya michezo na
vituo vya utangazaji jana Jijini Mwanza
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi
iPad afisa habari kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Stephen
Msengi wakati wa ziara ya yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia
jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa
mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji
vilivyopo jijini hapo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John
Mongella
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza
Meneja wa Star times kanda ya ziwa Bw. Bakari Hassani (kushoto)
alipotembelea ofisi hizo wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa
maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo
vya utangazaji vilivyopo jijini hapo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na
viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika uwanja vya CCM
Kirumba kupata taarifa ya uwanja huo wakati wa ziara yake kukutana na
wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa
habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya
utangazaji vilivyopo Jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Mwanza Ndg.
Miraj Mtaturu.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza


0 comments :
Post a Comment