KESHO Jumapili, Coastal Union itacheza
na Yanga mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Mkwakwani
mjini hapa, sasa tayari vitimbi vimetawala kabla ya mechi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa matawi
mbalimbali ya Yanga kutoka Dar es Salaam wakishirikiana na wenzao wa
Tanga, wanadaiwa kupiga kambi mkoani hapa kuweka mazingira ya ushindi
kwa timu yao.
Miongoni mwa mazingira hayo ni kusoma mbinu na hujuma zinazopangwa na Coastal katika mchezo huo ulioteka hisia za mashabiki wengi wa Tanga.
Viongozi hao wamepiga kambi katika hoteli kubwa zilizopo katikati ya jiji eneo la Chuda na kandokando ya Bahari ya Hindi eneo la Raskazone, wameingia kimya kimya bila watu wengine kufahamu.
Mmoja wa wanachama wa matawi ya Yanga mkoani hapa, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, viongozi hao wana wiki nzima jijini hapa wakipanga mikakati ya kuhakikisha timu yao inashinda.
“Mbona viongozi (hao wa Yanga) wapo Tanga muda mrefu tangu Yanga ilipokwenda Misri na wao wakapiga kambi mkoani hapa kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa Jumapili,” alisema mwanachama huyo kwa sharti la kutotajwa jina.
Alisema tayari wamepata vitu mbalimbali kutoka kambi ya Coastal Union na kilichobaki sasa ni utekelezaji uwanjani.
SOURCE: CHAMPIONI

0 comments :
Post a Comment