Moto wa Rais Magufuli waingia BAKWATA, Katibu wake atumbuliwa kwa ubadhirifu


MOTO wa rais Dk. Magufuli wa utumbuaji wa majipu umepiga hodi hadi kwenye madhehebu ya dini Mkoani Singida, baada ya Katibu BAKWATA wilaya ya Singida Vijijini, Salum Abrahaman Masaka, kutumbuliwa jipu/kusimamishwa kazi kwa nuda usiojulikana kutokana na tuhuma ya ubadhirifu wa shilingi 640,000 mali ya BAKWATA.
Akizungumza na Modewjiblog ofisini kwake, Katibu wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Singida, Alhaji Burhan Mlau, alisema Salum amesimamishwa kazi  kuanzia April 19 mwaka huu.
Alisema maamuzi hayo mazito na magumu, yametolewa na kikao halali cha halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.
 “Baadhi ya tuhuma zinazomkabili Salum ni pamoja na kusababisha hasara ya shilingi 640,000 ambayo ni amana na waislamu wa Singida vijijini,kudanganya Jumuiya ya akina mama kwamba angewapa gunia moja la mahindi na amekuwa akikusanya mapato ya usajili wa ndoa na  hajaziwasilishi kwenye mamlaka husika”,alisema.
Akifafanua, Alhaj Mlau alisema kutokana na tuhuma ambazo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi, imewalazimu wamsimamishe kazi, ili kupisha uchunguzi huo hadi hapo uamuzi mwingine utakapofanyika.
“kwa kifupi Salum amesimamishwa kazi baada ya halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini kukosa imani na utendaji wake wa kazi”, alisema.
Katibu huyo,alisema kwa sasa nafasi hiyo amekaimishwa Said Alli Mang’ola.
Wakati huo huo, Alhaji Mlau, ametoa wito kwa watendaji wa BAKWATA mkoani Singinda wawe waadilifu, waaminifu na kutunza vizuri mali ya waumini.
“Nikumbushe tu kwamba dini ya Kiislamu, ni dini ya kweli, imani, utulivu na haina kabisa nafasi ya viongozi wenye tama ya kujinufaisha binafsi na mali ya Waumini”,alisisitiza.
Hivi karibuni Askofu wa Kanisa la Pentekoste (FPCT) Jimbo la Singida Amos Maghasi, akifungua mafunzo  ya viongozi wanawake wa Kanisa hilo, alidai kuwa majipu hayapo serikalini  tu, yapo hadi ndani kwenye madhehebu ya dini.
Imeandaliwa na Nathaniel Limu, Singida
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment