BMT
yaagizwa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa viwanja vya michezo
vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii kwa ajili ya matumizi ya michezo.
Agizo
hilo limetolewa leo na na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nuru Khalifani Milao alipofanya ziara katika ofisi za
Baraza hilo kwa ajili ya kujionea hali ya utendaji katika baraza hilo.
Mhe.
Wambura alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi
yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na
kufanya shughuli kinyume na taratibu.
“Kama
ilivyo katika Ilani ya uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote
yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu
kikiwemo na kile cha Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema
Naibu Waziri.
Aidha
Wambura alihimiza Bmt kuhakikisha inahamasisha ushiriki wa wanawake
katika michezo kwa kuwa michezo ipo kwa ajili ya wote na kuongeza kuwa
mbali na mashindano michezo pia utumika kujenga afya za mwanadamu.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed
Kiganja alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo watahakikisha
wanapiga hatua katika kukuza sekta ya michezo kwani BMT ndiyo mkono
pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo kisheria.
Ata
hivyo alielezea changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu
yao kuwa ni kuwa ni ufinyu wa bajeti, upungufu wa wafanyakazi na
muingiliano wa Wizara mbili katika utekelezaji katika ngazi ya Manispaa
na Halmashauri Maafisa Michezo wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI
hivyo kuna haja ya kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kushirikiana.
Na: Frank Shija, WHUSM
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura akipokelewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Mohamed Kiganja alipofanya Ziara katik ofisi za Baraza hilo leo jijini
Dar es Salaam.Kutoka kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a
na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura aakizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
alipofanya Ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru
Halfani Mrisho Milao akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri
wa wizara hiyo Mhe. Annastazia James Wambura (katika) katika ofisi za
Baraza la Taifa la Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.
Katibu
Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura
(kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia
ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura, Naibu Katibu Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
Makoye Alex Nkenyenge wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa BMT
Mohamed Kiganja wakati wa ziara yake katika ofisi za Baraza hilo jijini
Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa BMT leo jijini
Dar.Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na wa
mwisho kulia waliokaa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Mohamed Kiganja.
Picha zote na: Frank Shija, WHUSM
0 comments :
Post a Comment