Kwa kipindi cha karne hii ya 21, vijana wenye umri wa chini wamekuwa watumwa wa mitandao ya kijamii, je nini hasara na faida zake?
Kumekuwa na kesi nyingi zinazoendelea kuhusu Internet Addiction Disorder( IAD), ambapo umekuwa ni ugonjwa unaokufanya usiweze  kukaa au kufanya kitu bila kupitia kwenye internet, hali hii imesadikika kuweza  kuangamiza kizazi kikubwa cha karne ya 21, na hasa kuleta matatizo katika  mishipa ya fahamu, matatio ya kisaikolojia na ya kijamii.
Matatizo ya mishipa ya fahamu yanapelekea hata kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria kwa haraka hasa pale unapokuwa upo makini katika kuperuzi simu yako, pia  kichwa kuuma kwa muda mrefu kwa kutumia muda mwingi katika simu yako na hata baadae kuchoka kiakili na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo .
Kisaikolojia inamuharibu kijana hasa katika uwezo wa kufikiri na kuwaza, anaweza kujihisi hawezi kukaa bila simu yake, hawezi kukaa bila kujua nani kafanya nini au afanye nini kuwaridhisha marafiki wa kurasa za facebook na Instagram, na hata kupelekea kuleta matabaka katika jamii watu kujuana kiundani na kutengeneza chuki kwa  baadhi ya watu au nchi, na hata kuleta kuigana katika mtindo wa maisha.
Watu wengi wamelalamika kuhusiana na kuaibishwa kupitia mitandao ya kijamii, lakini kwa baadhi ya nchi kama Tanzania kumekuwa na sheria za kuzuia matumizi mabaya ya internet.
Lakini pia, kwa upande wake Andrea Guzzoni ambaye ni Meneja Mkazi wa kampuni ya JovagoTanzania alifafanua kuwa, Matumizi ya tovuti yanafaida kubwa kiuchumi, watanzania hawana budi kuangalia suala hili kwa upande wa pili.
“Tutumie kurasa za facebok, Instagram na Twitter katika kujifunza mambo ya kimaendeleo na kutangaza biashara zetu, lakini pia serikali inabidi iwajibike katika kuzuia baishara za utapeli zinazoendelea ndani ya mitandao” aliongezea.
“Wapo waliofanikiwa kupitia hii mitandao na wapo wanaondelea kuharibikiwa kupitia mitandao hiyo hiyo, ni wakatai wa kubadilika na kutumia uhuru wa habari kwa manufaa yetu”. Lilian Kisasa, Meneja Mawasiliano  wa Jovago Tanzania aliongezea.