Ligi Kuu ya Uingereza usiku wa Jumatatu iliendelea kwa mchezo mmoja kati ya Tottenham na West Brom Albion ambapo ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Totttenham ilikuwa ya kwanza kupata goli baada ya beki wa West Brom, Graig Dawson kujifunga dakika ya 33 na baadae dakika ya 73 kusawazisha makosa na kuisawazishia West Brom goli na hadi dakika ya 90 wakatoka moja kwa moja.
Baada ya matokeo hayo, tofauti ya alama kati ya vinara wa ligi, Leicester City na Tottenham ni alama saba na michezo iliyosalia ni mitatu hivyo Leicester inahittaji alama tatu kutangazwa kuwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) 2015/2016.