Rais
John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hufanyika kila mwaka,
Aprili 26.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu,
Rais Magufuli amewataka wananchi kusherehekea siku hiyo kwa kupumzika
majumbani kwao na katika shughuli zao binafsi.
Aidha,
fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kugharamia vyakula, vinywaji,
gwaride na mengineyo ameagiza zielekezwe katika upanuzi wa barabara ya
Mwanza ‘Mwanza – Airport’, katika eneo linaloanzia Ghana Quarter hadi
katika uwanja wa ndege jijini humo, kwa lengo la kupunguza msongamano wa
magari.
Hii ni Taarifa Rasmi toka Ikulu
0 comments :
Post a Comment