Rais Magufuli Atoa shilingi Milioni 10 nyumbani kwao Geita Jana Kuchangia Upanuzi wa Kanisa


Rais Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa la bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchagia upanuzi wa kanisa hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo Jana tarehe 03 April, 2016.

Kabla ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao unaendelea.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia kuadhimisha miaka 50  tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao unachangiwa na waumini wenyewe.

Padre Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment