Na Rabi Hume, Mara
Kwa
kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto, Taasisi ya Graca Machel kwa
kushirikiana na serikali imefanya uzinduzi wa mradi ulio na malengo ya
kuwarudisha shule watoto 20,000 waishio mkoa wa Mara ambao hawakupata
nafasi ya kuwa shuleni.
Akizungumzia
mradi huo, Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel alisema
taasisi yake imeanzisha mradi huo kwa kutambua kuwa kuna idadi kubwa ya
watoto walio nje ya shule kwa sababu mbalimbali hivyo kupitia mradi huo
ni matarajio yao kuona watoto wakirudi shule ili kupata elimu ambayo
itawasaidia kwa maisha yao ya baadae.
Aliongeza
kuwa anatambua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere kwa kuacha msingi bora
wa elimu kwa watu wa aina zote na kuwataka wasimamizi wa mradi huo
kuhakikisha wanafanikisha mradi kwa kuweka usawa baina ya watoto wa kike
na watoto wa kiume ili wote wapate nafasi ya kurudi shule.
“Watoto
wanatakiwa wawepo shuleni na wapate elimu bora bila kufanya upendeleo
kwa watoto wa kike na watoto wa kiume ili wamalize pamoja elimu ya shule
ya msingi na kuendelea na masomo wote wafikie malengo yao,
“Tunataka
watoto wasio chini ya 20,000 warudi shule natambua Mwalimu (Nyerere)
aliweka msingi bora wa elimu na ni haki ya watoto wote kupata elimu,”
alisema Bi. Machel.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akizungumza jambo kuhusu mradi huo.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo aliishukuru Taasisi ya Graca
Machel kwa kupeleka mradi huo mkoa wa Mara na kuahidi kuwa atakuwa
kiongozi kufanikisha mradi huo ambao utafanyika kwa kipindi cha miaka
miwili.
Pia
alitumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa watumishi walio chini yake
kufanya kazi kwa juhudi katika maeneo yao pindi wanapohitajika kusaidia
ili kufanikisha mradi huo ambao una malengo ya kuwasaidia watoto wa mkoa
wa Mara kurudi shuleni.
“Nina
shukuru sana kwa kuletewa mradi huu na Taasisi ya Graca Machel na
nitashiriki kwa asilimia 100 kufanikisha mradi, na nitoe rai kwa
watumishi wenzangu kuwa wafanye kazi kwa bidii kuanzia sasa tufanikishe
mradi kama umevyopangwa,” alisema Mulongo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo akimshukuru mwanzilishi wa Taasisi ya
Graca Machel, Graca Machel kwa kupeleka mradi huo mkoani kwake.
Aidha
pamoja na kuzinduliwa kwa mradi huo, pia kunataraji kufanyika utafiti
kutazama ni changamoto gani ambazo zilikuwa zinasababisha watoto wa mkoa
huo kuwa nje ya shule, utafiti ambao utafanywa na Taasisi Huru ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
Akizungumzia
utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema
wanataraji kuanza kufanya utafiti kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
itafanyika mwezi huu Aprili na awamu ya pili itafanyika mwezi Julai.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akizungumzia utafiti unatarajiwa
kufanywa na ESRF kuhusu changamoto ambazo zilikuwa zinasababisha watoto
wa mkoa wa Mara kuwa nje ya shule wakati wa uzinduzi wa mradi ulio na
malengo ya kuwarudisha shuleni watoto 20,000.
“Utafiti
huu ambao unamalengo ya kufanikisha watoto 20,000 wa mkoa wa Mara
kurudi shuleni utafanyika kwa awamu mbili, unaanza Aprili kwa maeneo ya
Musoma, Bunda, Rorya, Butiama na Wilaya ya Tarime,
“Awamu
ya pili itafanyika kuanzia mwezi Julai kwa eneo la Manispaa ya Musoma,
Bunda Mjini, Tarime Mjini, Serengeti na Magumu,” alisema Dkt. Kida.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiweka saini ya kuashiria kufanyika kwa mradi huo.
Watiliaji saini ya makubaliano ya mradi huo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Baadhi
ya washiriki katika uzinduzi wa mradi huo, Wa kwanza Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Mwanzilishi wa Taasisi ya
Graca Machel, Graca Machel, Askofu Michael Msongazira wa Kanisa la
Roman, Musoma na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof.
Fortunata Makene.
0 comments :
Post a Comment