Rais
wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongoza ujumbe wa
maofisa wengine wawili wa shirikisho hilo wamefanya ziara makao makuu ya
ofisi za TBL Group zilizopo Masaki jijini ambapo walikutana na
mkurugenzi wake Mkuu Roberto Jarrin na kufanya naye mazungumzo.
Ziara
hiyo imeelezwa kuwa ina lengo la kudumisha uhusiano miongoni mwa
taasisi hizo mbili hususani katika kuendeleza mchezo wa soka nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL GROUP Roberto Jarrin (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa
Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa , Kulia ni Rais wa shirikisho la Mpira
wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi.
Rais
wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili
kulia ) Katibu Mkuu shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine (kushoto) na
Mjumbe wa Kamati ya TFF Richard Sinamtwa (katikati) wakimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin (Kulia ) wakati
walipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL GROUP, Roberto Jarrin (wapili kushoto) Rais wa shirikisho
la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kutoka
kulia) Katibu Mkuu shirikisho hilo , Mwesigwa Selestine (kulia) na
Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa (kushoto )wakiwa kwenye picha
ya pamoja wakati walipotembelea katika ofisi za TBL Masaki jijini Dar
es Salaam.


0 comments :
Post a Comment