Wabunge
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya
Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu
shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha
ya kumiliki asilimia 20% ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha Tanalec
kilichopo jijini Arusha .
Kamati
hiyo ya Bunge imebaini hayo wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda
jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda
ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua
transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya
,Zambia Malawi na Burundi.
Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo alisema
kuwa ni jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa Tanalec na
wako katika wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza transfoma nje ya
nchi suala ambalo linapaswa kutazamwa kwa umakini na kupatiwa majibu.
“Tunashindwa
kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao na
wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba yuko ndani ya bodi ya
wakurugenzi ,hapa kuna mgogoro ambao unapaswa kuatatuliwa kwa wakati
ili kunusuru kiwanda hiki” Alisema Lema
Naye
Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa Tanesco
kununua transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji wa viwanda vya
ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda
nchini kwani ni vigumu kukuza viwanda wakati bila kuvilinda viwanda vya
ndani dhidi ya bidhaa za nje.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vicky Kamata na Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua maamuzi juu ya suala hilo la
Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze kuchochea maendeleo ya
Taifa.
Meneja
Mkuu wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali irekebishe sheria za
manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze kukua na
kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.
0 comments :
Post a Comment